Monday, January 28, 2008

Mauaji ya Kutisha Kenya

Afrika mashariki inaundwa na nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Nchi hizi zinaishi kwa Amani na Utulivu. Pamekuwepo na ushirikiano wa kuridhisha baina ya nchi hizo: Kiuchumi na Kisiasa.

Mwaka jana 2007 Kenya ilifanya uchaguzi wake mkuu ambapo Raisi Mwai Kibaki alimshinda mpinzani wake mkubwa Ndugu Raila Odinga wa ODM. Ushindi huo uliomtangaza Mwai Kibaki kuwa Raisi uligubikwa na ghasia za hapa na pale kutokana na kile kilichosemwa kwamba Mwai Kibaki aliiba kura.

Wananchi wengi wasio na makosa au hatia (wanawake, watoto, vijana na watu wazima) wameuawa na bado mauaji yanaendelea. Vitendo vya ubakaji, wizi wa kutumia nguvu na uchomaji mali ovyo bado vinaendelea.

No comments: