Monday, September 24, 2007

UMUHIMU WA KUWEKA MAZINGIRA YETU SAFI

Ni ukweli usiofichika kwamba mazingira yanapokuwa safi huvutia macho. Na ni kinga tosha ya magonjwa kwani wadudu kama mbu watakosa mahali pa kuzalia. usafi huanzia tunapoishi. Kusafi na kudeki nyumba zetu kila wakati. Kufagia mazingira kuzunguka nyumba zetu na kupanda maua na kuyatunza. Haya yote hufanya mazingira yetu kuwa na muonekano mzuri.
Cha kushangaza au sijui nisemeje ni kukuta mtu ni msafi awapo njiani au kazini, ukifanikiwa kufika anapoishi unaweza kushangaa, kwani hakuna tofauti na jalala la Tabata. Pia ofisini ni pasafi kiasi kwamba unaweza kuvua viatu na kuingia peku. Je ni kwanini huwa hivyo?