Sunday, October 12, 2008

Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja

Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja husababishwa na tamaa. Ndio sababu wasichana wengi wadogo wana simu za bei kubwa ukilinganisha na watoto wa kiume hata kuliko sisi wazazi. Wakiume pia wapo kwani wapo wachache ambao wanamilikiwa na mashuga mami, ambao huwaita Serengeti boys. Utakuta mtu ana rafiki kwa ajili ya lift, mwingine kwa ajili ya chips na vinywaji, yupo wa kwenda nae beach na kadhalika. Sisi kama wazazi inabidi tubadili mwelekeo na mtazamo, tuache kushabikia tunapoona mtoto wa jirani au ndugu anapotoka.

Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja ni tatizo kubwa sana, linahitaji ujasiri wa hali ya juu. Na elimu ya ziada inatakiwa kutolewa. Kwani kuna wingi wa demokrasia ya vyombo vya habari ambavyo vinachochea mtu kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja. Pia heshima ya woga ndani ya wapenzi ni sababu kubwa ya tatizo hilo. Mmoja anaogopa kumwambia mwenzake abadili staili ya mapenzi kwani anaogopa kuonekana mhuni. Na pia anafikiria iwapo ataniktalia nitajisikiaje? Vibanda vinavyoonyesha mikanda au video usiku navyo ni chanzo kikubwa sana, kwani ufikapo usiku mnene mikanda yenye vishawishi vya ngono huonyeshwa. Fungakazi ni kwenye internet na kwenye simu. Kwani watu wanatumiana move za kutisha za kimapenzi kwenye simu. Nyumba za wageni nazo hazichagui, ili mradi ulipie. Uingie na mtoto wa sekondari, wa shule ya msingi, wa chuo na kadalika hakuna wakukuuliza, je tutafika?

Elimu na ushirikiano vinatakiwa. Femina mna kazi nzito ya kufikisha ujumbe kwa walio wengi hasa vijijini. ONE LOVE IS A SOLUTION.

Kipindi cha Fema wiki hii kililenga panapostahili, pale kijana kutoka Mtwara alipokiri kuwa rafiki zaidi ya mmoja wa kingono. Kitendo hicho kilimpelekea kijana huyo kupata gonjwa la ngono. Cha kushangaza ni kwamba kijana huyo hakujua gonjwa hilo alilipata kutoka kwa mwanamke yupi? Nilichojifunza ni kwamba, vijana tulio wengi hatutaki kutumia kinga na tunachukulia magonjwa ya ngono ukiwepo UKIMWI kama ajali kazini. Mahusiao ya kingono kwa mpenzi zaidi ya mmoja ni hatari sana.

Bwana ishi na tuli wake walitoa ujumbe mzito sana.