Thursday, September 11, 2008

UNYANYAPAA NA VIRUS VYA UKIMWI

Nilisikiliza kipindi cha Femina Talkshow cha wiki hii kwa masikitiko makubwa sana. Kuna dada mmoja mlemavu alipata ukimwi na kutelekezwa na familia yake. Mwanadada huyo aliamua kueleza wazi kuwa ni muadhirika akitegemea kupata msaada kutoka kwa familia yake. Chakushangaza ni kwamba alinyanyapaliwa na kutengwa na familia yake. Kwa sasa analelewa na mtu aliye wa familia yake. Ni ndugu wa kutoka kijiji kimoja. Mambo kama hayo yapo kwenye familia nyingi. Ndio maana tulio wengi tunaogopa kujitangaza. Kwani kujitangaza ni kunyanyapaliwa na jamii na pia kutengwa. Huyu mlemavu alijitoa mhanga na kujitangaza. Alikuwa na ujumbe mzito kwa wa-Tanzania. Kwani tulio wengi tunadhani walemavu hawana ukimwi? Dunia imebadilika. Hakuna mlemavu, watoto wa shule wala nani. Wote wanao. All are vulnerable to HIV/AIDS.

Ni wajibu wetu kama jamii kuwahudumia waadhirika wa ugonjwa huu kwa hali na mali. Kwani wote ni watarajiwa wa ugonjwa huo. Nilisoma jana kwenye jamii forums kwamba kuna mtoto alikuja papai na kupata HIV. Uchunguzi ulipofanyika uligundua kwamba aliyemuuzia mtoto huo papai alikuwa na jeraha liliokuwa linatoa damu. Kwa hali hiyo mtoto alipata ukimwi kwa nia hiyo. No one is safe against this killer disease.
Ninatoa pongezi kwa kipindi cha Femina Talk Show hiki kwani kinatoa mambo muhimu yanayozikumba jamii zetu. Kwa hiyo tujifunze kupitia kipindi hiki.

No comments: