Monday, September 8, 2008

Bei ya Nyama Jiji Dar Sasa Inatisha

Maisha ya mwananchi wa kima cha chini yanakuwa magumu siku hadi siku. Wiki iliyopita bei ya nyama ilikuwa ni shilingi 3,200 kwa kilo kwa fedha ya ki-Tanzania. Juzi nilinunua nyama hiyo hiyo kwa shilingi 3,400 kwa kilo. Cha kushangaza ni kwamba leo asubuhi nimenunua nyama kwa shilingi 3,600 kwa kilo moja. Je tutafika?
Ninachojiuliza ni kwamba wakati wa mfungo Mtukufu wa Ramadhani nyama inatumika kwa wingi sana au tatizo lipo wapi? Nikiangalia sioni sababu ya kufanya nyama ambayo ni kitoweo muhimu kwa wananchi kupanda hasa wakati wa sikukuu kubwa kama hii ya Mfungo, X-Mass na Pasaka. Ninadhani kuna haja ya kufanya juhudi za ziada ili kutuokoa sisi wa-Tanzania

No comments: