Thursday, September 18, 2008

MISITU NI DAHABU

Misitu ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu. Hutupatia dawa, kuni, mkaa na mbao. Misitu pia huvuta mvua, hutoa kivuli kwa ajili ya kupumzika pia misitu ni makazi ya wanyama. Faida hizi zote huweza kutoweka kwa muda mfupi iwapo matumizi hayatakuwa endelevu.

Uvunaji wa mazao ya misitu usioangalia na kukifikiria kizazi kijacho, huo in uharamia wa misitu. Uharibifu wa misitu umjitokeza sehemu mbalimbali hapa nchini. Mfano dhahiri ni misitu ya RUVU KUSINI. Misitu hiyo hukatwa kwa matumizi ya mkaa, kuni na mbao. Msitu huu umekuwa kama hauna mwenyewe. Chakushangaza ni kwamba msitu huu ni wa hifadhi ya Taifa.

Wananchi wanoishi karibu na msitu huu wanasema kwamba hawaoni umuhimu wa msitu huu kwao, kwani hawaoni faida nyingine tofauti na nilizozieleza hapo juu. Siku za nyuma walikuwa wakiulinda na kukamata maharamia pamoja na mazao waliyovuna msituni. Mazao hayo yalikuwa kama mbao, magogo ya kujengea, mkaa na kuni. Mazao hayo yalichukuliwa na serikali kuu pasipo kubakiza chochote katika kijiji. Mali iliyokamatwa iliuzwa kwa fedha nyingi sana lakini hakuna chochote kilichorejeshwa kwa wananchi au kijijini. Kwa sababu hiyo wananchi wakaamua kuacha watu wajivunie msitu kama wao.

Tatizo la yote hayo ni kutowashirikisha wananchi katika ulinzi wa misitu. Wananchi washirikishwe kwenye ulinzi wa misitu na faida zitokananzo na mazao ya misitu zigawanye kwa makubaliano ya wananchi. Sheria zitungwe au zitumike kuwaadhibu wanatumia misitu kinyume na taratibu. Pia wananchi waleimishwe umuhimu wa misitu na matatizo ya kutokuwa na misitu.

No comments: