Je tutafika? Leo nimesikia kwenye vyombo vya habari kuwa asilimia arobaini ya bidhaa zinazouzwa hapa nchini ni feki, zisikuwa sahihi kwa matumizi ya binadamu. Hii hali imenishtua sana. Kwani ni vigumu watu au watanzania tulio wengi kugundua au kujua kitu ambacho ni FAKE au GENUINE. Zinahitajika juhudi za ziada kuwaokoa wa-Tanzania. Kinyume na hapo tutalipoteza taifa hili.Cha kujiuliza, hizo bidhaa feki hadi kufikia asilimia arobaini zinaingiaje nchini? TRA wananfanya nini? TBS wanafanya nini? Wafanyakazi mipakani, viwanja vya ndege na bandarini wanafanya kazi gani? Hayo ni maswali ambayo sina majibu la haraka. Je nini kifanyike. Nchi inanuka rushwa. Maisha ya wananchi yapo hatarini.
This ad zapped.
Saturday, September 6, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment