Ni ukweli usiofichika kwamba mazingira mazuri yanavutia watu kuishi. Lakini kuna watu wasioona umuhimu huo. Ukitembelea maeneo ya Manzese utashangaa kwani ni kawaida kuamka asubuhi na kukuta furushi la taka mlangoni mwako au kuzunguka nyumba yako. Unajiuiza hawa watu wana akili timamu au la. Nimejaribu kuwauliza na watu wachache, majibu yao yalikuwa ya kukatisha tamaa. Wengine walisema hizo taka niliziweka mimi, wengine wakasema hawaoni ni kwa nini watupe hapo wakati kuna sehemu ya kutupa hizo taka.
Kila la heri wana-blogu
Thursday, August 2, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Vipi kuhusu vibaka,kelele usiku,purukushani za wezi watu sio kero huko tupe uhondo
Karibu Mkuu!
Tuko Pamoja!
Post a Comment