Monday, August 6, 2007

MANZESE MPYA SEHEMU YA PILI

Kwa walio wengi wetu wanaweza wasiamini. Ila ni ukweli usiofichika kwamba kwa biashara, eneo la Manzese kumekucha. Ni aghalabu sana kuona eneo hili likiwa tupu bila watu. Eneo hili lipo bize wakati wote mchana hadi usiku. Wapo wanaotoka makazini, kwenye biashara zao, na wafanyabiashara wanaofanya biashara eneo hili la Manzese. Pia wapo wanaotoka kwenye starehe baada ya kazi ngumu za mchana.
Biashara kubwa iliyopo eneo hili ni ya KUSAGA na KUKOBOA NAFAKA, asilimia kubwa ikiwa ni mahindi. Unga ni chakula kikuu hasa hapa Dar es Salaam, kwa kiasi kikubwa unga huo unatoka eneo hili la Manzese. Je! Manzese si mahala pa kupaheshimu sasa? Muda wote wa siku masaa 24 mashine ya kusaga nafaka zinafanya kazi. Biashara/kazi hii imetoa ajira ya moja kwa moja kwa wananchi walio wengi, kwa waendesha mashine na wanaosafisha na kuchambua hizo nafaka kabla ya kusaga au kukoboa. Pia wafugaji wanapata pumba kwa ajili ya mifugo yao kama ng'ombe, mbuzi, nguruwe, kuku, n.k. Kilicho na faida hakikosi matatizo au lawama. Tatizo kubwa ni makelele yanayotokana na machine hizo pamoja na vumbi la nafaka.
Pia zipo biashara kubwa na ndogo ndogo kama maduka ya jumla, maduka ya watu binafsi ya vyakula na ujenzi. Pia zipo Bar, Groceries, maduka ya dawa, uuzaji wa vifaa vilivyotumika (used equipments), n.k.
Asanteni kwa kusoma.

1 comment:

luihamu said...

Hii safi sana mkuu.naona unakasi ile mbaya natumai mwendo ni ule ule,kaza buti,tupashe zaidi.