Sunday, August 5, 2007

MANZESE MPYA

Manzese ni sehemu ambayo watu wengi wana mawazo kwamba si mahala pazuri pa kuishi. Siku hadi siku maeneo mengi ya Manzese yanaboreshwa ikiwemo Manzese Uzuri eneo ambalo nimeishi toka mwaka 1995 hadi sasa ninapoandika NEWS hii. Uboreshaji wa Manzese ni kutokana na juhudi za wana-Manzese, ufadhili wa Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia (World Bank).
Barabara inayopita eneo hilo imejengwa kwa kiwango cha lami. Barabara za mitaa ndio sasa zinawekwa kokoto ili ziweze kupitika kwa muda wote wa mwaka bila matatizo yoyote.

Kilichokuwa kilio cha wakazi wengi wa eneo hili la Manzese ni MAJI. Miundo mbinu ya maji ndio sasa inakamilika. Na baada ya muda mfupi tatizo la maji katika eneo hili litakuwa ni historia.
Eneo hili la Manzeze halipo nyuma katika maendeleo ya elimu. Shule za msingi zipo za kutosha. wanafunzi wamalizapo elimu ya mzingi lengo lao ni kwenda sekondari. Wana-Manzese nikiwa mmoja wao tuliliona hilo na kuoa michango ya fedha, nguvu zetu n.k., kwa sasa eneo hili lina shule moja ya secondari inayoitwa Mazese Secondary School.
Baadae nitaelezea maendeleo katika sector ya biashara, nyumba za ibaada n.k. See you next time.
Karibuni Manzese mjionee maendeleo kwa ujumla.
Mhache

1 comment:

luihamu said...

Hii habari safi sana,inavutia kwani wengi tunaopenda kuhamia manzese huwa tunakuwa na shauku,manzese mmesikia,hii ni manzese mpya si ya kipindi ile.