Maisha ni mlima na ni kitendawili. Katika maisha kuna makundi mengi ya maisha kutokana na tafsiri ya mtu na vigezo alivyojiwekea. Kuna wale wenye maisha ya juu maisha ya kifahari. Kundi hili lina ishi kwenye nyumba nzuri, lina usafiri wa ghali na lina ulinzi wa mali zake. Wengi wa kundi hili wanaishi kwenye nyumba za serikali au wanalipiwa kodi na huduma nyingine kama maji, umeme n.k. na serikali au mashirika mbalimbali.
Pia kuna kundi la pili ambalo linaishi maisha ya kati, hili ni kundi ambalo chakula si tatizo kwao. ila halina kipato kinachowawezesha kuishi maisha ya juu. Kundi hili linaweza kuwa na nyumba bali huduma kama maji huw ani tatizo mara nyingine. Wachache wana nyumba zao.
Kundi la mwisho ni lile lenye maisha magumu. Kupata chakula au mlo mmoja kwa siku ni shida. kundi hili linaishi kwa kudra za mwenyezi Mungu. Kulala na njaa si tatizo kwao. Kwa upande wa mjini kundi hili huishi kwenye nyumba za kupanga na hasa kwenye yale maeneo ambayo huduma muhimu kama maji ni shida.
Je! Maisha si kitendawili?
No comments:
Post a Comment