Sunday, August 12, 2007

KITI-MOTO

Nguruwe ni mnyama anayefugwa. Hutembea kwa miguu minne. Mnyama huyu kwa watu ana fikra mbili. Moja kulingana na imani ya watu ni mnyama aliyekatazwa na MUNGU au na maandiko kuliwa kama kitoweo. Kwa upande wa pili ni chakula kizuri na nyama yake ni tamu sana.
Pamoja na fikra hizo, mnyama huyu hutoa faida zifuatazo kwa binadamu:
1. Nyama ijulikanayo na wengi kama "KITIMOTO"
2. Mbolea kwa ajili ya mazao
3. Kipato (income) kwa wafugaji wawauzapo hupata fedha pia wasafirishaji.
4. Ajira kwa wachinjaji na wauzaji wa jumla na rejareja
Week-end hii nilitembelea maeneo ya Mbezi Inn na kupata kinywaji bar moja iitwayo Green Park View. Bar hii ina sehemu ya kuuzia vinywaji kama beer, soda n.k. Pia wanatoa huduma ya chakula, chips, ndizi (za kukaanga na choma), nyama choma ya mbuzi, ngombe na kitimoto. Kitimoto hupikwa kutokana na matwaka ya mteja. Kwani kuna nyama ya Ku-Roast na kawaida iliyokaangwa tu. Na wengine huja kununua na kupeleka majumabni mwao.
Kwa utafiti wangu usio-rasmi "observation and participatory"niliona zaidi ya asilimia 70 ya wateja wanaoenda eneo hilo ni kupata "kitimoto" na wala sio kinywaji. Nilibahatika kuongea na mwenye mradi huo wa kitimoto na kunieleza kwamba biashara hiyo imemjengea heshima katika jamii. Kwani ameweza kujenga nyumba mbili zenye thamani kubwa, moja hapa mjini na nyingine Moshi Vijijini maeneo ya Kiboriloni. Pia anawasomesha watoto wake katika shule za msingi na secondary. Biashara hiyo pia imemjengea marafiki wengi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na nje ya nchi. Mwisho biashara hii inampatia mlo wa kila siku bila tatiza lolote. Kwa ujumla maisha ni mazuri kwake.
Karibuni eneo hili muone hayo niliyoyaainisha hapo juu.
Asanteni kwa kusoma.

1 comment:

luihamu said...

Safi sana,kazi yako inavutia na kuelimisha.