Mimi ni mmoja wa Wahadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania). Ni chuo kinachotoa elimu yake kwa njia ya masafa yaani Distance Education. Unapata elimu popote pale ulipo hapa Tanzania, haijalishi upo kijijini au mjini. Wengi wamejiunga na wamehitimu na kupata kazi nzuri kila pembe ya Tanzania na hata nje ya nchi.
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kipo wapi? Makao makuu ya chuo hiki yapo Tanzania, jijini Dar es Salaam katika wilaya ya Kinondoni. Ni chuo chenye mtandao nchi nzima. Kila mkoa una ofisi yake.
Ukitaka kujua zaidi kuhusu Chuo Kikuu Huria cha Tanzania soma kupitia www.openuniversity.ac.tz.
Karibu usome ukiwa unaendelea na majukumu yako.
2 comments:
Hello,Mhache, thankx for information, kama nataka kusoma pHD ya Demography hapo kwenu ipo.
Thank you
Post a Comment