Leo tarehe 11/02/2008 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kutangaza Baraza lake jipya la Mawaziri. Baraza la mawaziri lilivunjwa kutokana na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Ndg. Edward Lowasa kuachia ngazi kutokana na kuhushishwa na ufisadi wa Kampuni hewa ya Richmod.
Raisi wa Tanzania ameshamchagua Waziri Mkuu Mpya ambaye ni Ndg. Mizengo Pinda. Waziri Mkuu Mpya aliapishwa jumamosi tarehe 10/2/2008
Inatarajiwa na wananchi walio wengi kuwa Raisi atalipunguza baraza lake la mawaziri kutoka mawaziri 29 na manaibu mawaziri 31 na kuwa na baraza dogo zaidi.
Monday, February 11, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment